4 Mei 2016 - 17:57
 Jenerali Qasim Suleimani aonekana katika viwanja vya mapambano nchini Syria

Jenerali wa jeshi la Qudsi (Qasim Suleimani) ameonekana nchini Syria katika mkoa wa Halab akiangalia kwa karibu mapambano ya wanajeshi wa Syria dhidi ya magaidi nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda huyo katika masiku ya hivi karibuni alionekana katika viwanja vya mapambano nchini Syria akiangalia maendeleo ya mapambano dhidi ya magaidi hao, na kutathmini hali ya mwendelezo wa ukombozi wa maeneo yanayokaliwa na magaidi nchini humo.
Kamanda wa jeshi la Qudsi akiwa na makamanda wengine wa jeshi hilo toka zilipoanza vurugu na machafuko ya Syria, mara nyingi wamekuwa wakihudhuria katika nchi hiyo, na kutoa ushauri wa lazima wa mapambano hayo dhidi ya magaidi nchini humo.
Kadhalika jeshi la Qudsi pia limekuwa likionekana nchini Iraq katika kupanga mbinu za kuyakomboa maeneo muhimu yaliotekwa na magaidi wa kikundi cha Daesh.
Ushiriki wa makamanda wa jeshi la Qudsi nchini Iraq na Syria kumezungumziwa sana na wataalamu wa masuala ya kijeshi duniani huku wakimtaja Jenerali Qasim Suleimani kuwa ndio kichwa na msingi muhimu katika kupanga mashambulizi ya kijeshi katika nchi hizo ambapo emesaidia kusitisha kasi ya za magaidi kuteka miji muhimu ya nchi hiyo.
mwisho wa Habari/290